Habari!
Leo niko na habari tofauti kidogo, Tangu ninunue modem kutoka zain nimekuwa nikifurahia huduma zake mno kiasi ya kusema kuwa sina haja ya kununua modem za mitandao mingine, ila kuna kitu sikukiweka akilini mapema. Si muda woote nitakuwa nikiunganishwa, hivyo mara nyingine tena mara kwa mara huwa nakosa huduma ninapoihitaji na wazo hunijia pengine ningekuwa na modem za mitandao tofauti basi ningekuwa na swichi tu.
Kuna njia mbadala kwenye hilo, nikaanza kufuatilia fuatilia kwenye wavuti, nikapata namna ambayo nitaelekeza kupitia ukurasa huu. Na kwa kukumbusha tu ni kwamba, inaweza ikakusaidia au isikusaidie kutokana na kuwa zoezi zima ni la kujaribu kwa nia ya dhati ukiwa tayari kwa matokeo yoyote. Binafsi sikuwa na cha kupoteza wala kusubiri, na kama wengine walijaribu na wakafanikiwa kwa nini mimi niogope au nishindwe. Kama uko na roho/misimamo kama hiyo basi fuata maelekezo haya:-
nenda hapa http://www.bb5.at/huawei.php?imei=<IMEI yako hapa > kama utashindwa kwa njia hiyo hapo, basi inabidi utafute kikokotoo kingine, mimi nilijaribu hiki http://www.mediafire.com/?myfd1zd1cnt kama bado kitashindwa kufanya kazi basi jaribu ku google kwa kutumia model ya modem yako.
Niweke kitu kimoja sawia hapa, kuna modem ambazo zinatumia software inayoitwa MOBILE CONNECT isipokuwa zile za VODACOM kwa hapa kwetu Tanzania. Hizo za mwanzo unachotakiwa ni kuingiza line ya mtandao mwingine tofauti na ulionunulia modem hiyo, Mobile Connect itashindwa kuitambua na hivyo itaomba Unlock code na kutoa majaribio 10 bila shaka, utaingiza namba utakazo zipata kutoka kwenye programu hiyo uliyoishusha ikiwa ulliweka IMEI sahihi ya modem yako.
Kwa wale wengine ambao hawana Mobile Connect watahitajika kutumia http://www.sagmaster.com/download/10SMTi/HUAWEI_MODEM_Code_Writer.rar kupeleka unlock code kwenye modem yako.
Michezo hii yote nmeifanya kwenye modem yangu ya HUWAWEI E1550, kwa wenye model kama hii, nauhakika itakubali tu, tofaui na apo pia nitakuwa nimetoa njia mbadala, unachohitaji ni ku google kwa kutumia jina na model ya modem yako ipasavyo na tangu hapo nimekuwa nikibadilisha line za mitandao tu bila wasiwasi, inanisaidia sana!.
Karibu na Ufurahie tekinolojia.
BBKisaki a.k.a BlacSko.
March 22nd, 2011 at 8:44 pm
ur work is so greaty..
April 26th, 2011 at 9:07 pm
Dah kwanza hongera kaka kwa kazi nzuri ka hii, web imetulia mbaya ka mbele vle. tuachane na hyo, hata mm nilijulia ukouko kwenye hyo site ulioitaja hpo juu na nilijaribia kwenye modem ya zain huawei 1550,ila bdo cjajua kuunlock modem za vodaphone ndo natafuta nikipata 2tashea na wadau wa hii site. afu bgup sana kwa kuwahimiza wana wajitume watu wanataka mabadikiko lkn hawako tayari wao kubadilika, pamoja kaka kla la kheri…
April 27th, 2011 at 1:50 pm
Nashukuru Adolph, hii ni fani yetu na ni wajibu wetu kuendeleza ili TZ iwe sawa kivile.
Vodaphone wao hutumia modem zinazotengenezwa na ZTE Corporation si huwawei, waweza kunitumia model yake nami nitakusaidia ipasavyo.
Endelea kupitia mtandao huu tafadhali…
May 1st, 2011 at 8:19 pm
how abt modem zisizotumia sim card like zantel modem
May 2nd, 2011 at 10:26 am
Canho, kila modem ina sim card, hizo za zantel zinazo ila zimetengenezwa kwa mtindo utakaokupa shida kufungua na kutoa sim card mara kwa mara, hivyo hata mimi sikushauri sana lakini unaweza ukajaribu kwa msisitizo na ili ufurahie pengine itakubidi uwe waiachawazi kwa matumizi fulani fulani.
Zantel pia wanatumia za ZTE Corporation sawa na vodacom ila design zao ziko tough kuzifunguafungua.
July 19th, 2011 at 9:57 pm
hey bro hapa nina modem ya huaweiE153 ya Tigo ila niki2mia line ya mtandao mwingine it doesnt give me tha option of entering the unlock code so wat shud i do?..b’coz tigo is too expensive in case of rechargin bundles..in deeply need ur assistance bro..
July 20th, 2011 at 3:34 pm
Steven, samahani kwa kuchelewa kukujibi!
Kwa hiyo modem yako ya tigo, kama hailuzi unlock code then, try to connect with it ila itakataa kwa sababu unatumia mobile connect amabayo inatambua line za tigo tu, nakushauri upitie hapa baada ya two days u’ll find a link that u can download Mobile connect which is for general use!